Yanga, Simba waigombania saini ya 'mido' ya Coastal
Sisti Herman
May 12, 2024
Share :
Klabu kubwa na kongwe za Tanzania, Yanga na Simba zipo kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa kati wa klabu ya Coastal Union Greson Gerald Gwalala "Tripple G" ambaye amekuwa na kiwango kikubwa akiwa na Mangushi msimu huu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya Coastal Union klabu hiyo inakaribisha makubaliano ya kibishara na timu hizo za Kariakoo.