pmbet

Yanga vs Medeama ni "GSM DAY" - Ali Kamwe

Sisti Herman

December 17, 2023
Share :

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Ali Kamwe, leo kwenye mkutano na waandishi wa habari amethibitisha kuwa katika kuhamasisha siku ya mchezo wao wa raundi ya 4 wa ligi ya mabingwa ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Medema wameupa jina la "GSM DAY" katika kuendeleza utamaduni wa kuwapa wachezaji na watu muhimu siku za michezo yao ya kimataifa

“Tumekuwa na kawaida ya kuwa na siku za wachezaji, sasa tumekuja kiutofauti, mdhamini na mfadhili wetu Ghalib Said Mohamed amenunua tiketi zote za mzunguko. Hivyo mechi ya Medeama FC tunakwenda kwa jina la GSM Day kuthamini mchango wake kwenye mchezo huu” Ally Kamwe

“Je kwenye siku ya GSM Day tunatokaje? Ili kuheshimisha siku ya tajiri? Namna pekee ya kumuonesha tunathamini mchango wa GSM, siku ya jumatano hakikisha unakuja na jezi ambayo imetengenezaa na GSM. Ukija na jezi chupli hutaruhusiwa kuingia uwanjani.” Ally Kamwe

Fuatilia zaidi taarifa hii kwa undani kwenye mtandao wa Youtube wa PMTV

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet