pmbet

"Yanga wameleta barua na kuondoka" Afisa Habari wa TFF.

Joyce Shedrack

June 11, 2025
Share :

Afisa Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Nchini Cliford Ndimbo ameshangazwa na klabu ya Yanga kutokukubali kuzungumza na mamlaka hiyo ya soka juu ya sakata la madai ya fedha zao za ubingwa.

Cliford Mario Ndimbo (@ClifordMario) / X

Akizungumza muda mfupi baada ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Yanga kuwasilisha barua ofisi hapo na kuondoka Ndimbo amesema hizi ni taasisi kubwa sio kila jambo wanapaswa kuandikiana barua.

 

“Klabu ya Yanga wao wamefika hapa TFF wameleta barua na kuondoka na wamesema hawana chochote cha kuzungumza na sisi na hata Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alipomuita CEO wa Yanga wazungumze alikataa, hizi ni taasisi kubwa na sio kila jambo tunapaswa kuandikiana barua kama tunatoa posa”.
 

"Kama CEO wa Yanga SC hajui bingwa anapata nini kwanini wanasema wanadai kiasi hicho cha fedha wanachosema."- Cliford Ndimbo Afisa Habari wa TFF.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet