Yanga wampa Mshery mitatu mingine
Sisti Herman
July 5, 2024
Share :
Golkipa namba mbili wa Yanga, Aboutwalib Mshery amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.
Yanga imethibitisha kuwa kipa huyo amesaini mkataba baada kukaa mezani na na kufikia makubaliano Jana na Leo kusaini.
Mshery ailisajiliwa na Yanga kutoka Mtibwa Sugar Desemba 2021 na kuwa mchezaji wake mpya wa pili katika dirisha dogo baada ya kiungo fundi, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutoka Azam FC.
Kipa huyo amekuwa chaguo la pili chini ya makocha Nasreddine Nabi na Miguel Gamondi kutokana na ubora wa Djigui Diarra ambaye amekuwa chaguo la kwanza.