Yanga washusha chuma kingine kutoka Mashujaa FC
Sisti Herman
July 21, 2026
Share :
Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi aliyekuwa beki wa kati wa Mashujaa FC, Mohamed Musa kuwa mchezaji wao mpya.

Beki huyo ambaye pia anakipiga katika timu ya Taifa ya Zanzibar anakuwa mchezaji wa tatu kutambulishwa na Yanga kutoka Mashujaa baada ya Hussein Mihambo na Abdulnassir Assa 'Gamal'





