pmbet

Yanga watua kwa Madiba kwa kishindo

Joyce Shedrack

April 2, 2024
Share :

Klabu ya wananchi Young Africans imewasili kwa Madiba nchini Afrika Kusini mchana wa leo kwaajili mchezo wa marudiano dhidi ya Mamelodi Sundowns.

 

Wananchi wamepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana ambaye amepata nafasi ya kuzungumza na kikosi cha Yanga SC pamoja na benchi la ufundi akisema wana imani ijumaa Yanga inaenda kuliheshimisha Taifa.

 

Baadhi ya watanzania wanaoishi Afrika Kusini wamejitokeza kuwapokea kuanzia uwanja wa ndege wa OR Tambo wametoa ahadi ya kwenda uwanjani siku ya mchezo na kuishangilia timu ili iweze kuvuka hatua inayofuata.
 

Msafara wa Yanga SC tayari umeanza safari kutokea Jiji la Johannesburg Afrika Kusini kuelekea Pretoria ambapo mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns utachezwa.

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet