Yanga wawakabidhi Simba kwa Wazee
Sisti Herman
April 15, 2024
Share :
Meneja wa idara ya habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wamewapa wazee mechi ijayo ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Simba kama ambavyo walifanya kwenye michezo yao mikubwa ya ligi ya mabingwa Afrika kama Pacome Day, Aziz Ki Day, Max Day, Bacca Day na zinginezo.
"Kwa kutambua ukubwa na umuhimu wa mchezo wa Jumamosi, sisi kama Yanga tumeamua mchezo huu tunaukabidhi kwa wazee wetu, kwa hiyo ni Wazee Day, Wazee wangu wa Yanga, tumeuleta kwenu mchezo huu kama nafasi ya kuwaheshimisha, tukifungwa ni nyie, slogan yetu ni Wazee Day, mapigo ya kiutu uzima" alisema Ali Kamwe
Mchezo huo utachezwa wikiendi ijayo ya Aprili 20 kwenye dimba la Mkapa.