Yanga wazindua jezi na kuipiga dongo Simba
Sisti Herman
August 24, 2025
Share :
Mabingwa mara nyingi zaidi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wamezindua jezi za msimu mpya wa 2025/2026.
Yanga wamezindua jezi hizo pamoja kuziuza katika maduka ya GSM na Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Jangwani Jijini Dar es Salaam.
Yanga imezindua jezi zote tatu, moja jezi ya nyumbani na jezi nyingine mbili za ugenini.
Katika jezi hizo za Yanga kuna mahala wameandika tarehe 8/3/2025 siku ambayo walitakiwa kucheza na Simba, lakini Simba haikuleta timu, huku wakiongezea na walisepa.