pmbet

Yanga wazindua tawi Sauzi

Sisti Herman

April 4, 2024
Share :

Klabu ya Yanga chini ya Kurugenzi ya Masoko, wanachama, mashabiki ya klabu hiyo wamezindua tawi la wananchama wa klabu hiyo nchini Afrika kusini uzinduzi ambao ulihudhuriwa na Rais wa Yanga Eng. Hersi Said, Mwenyekiti wa DRFA Lameck Nyambaya, Mkurugenzi wa Masoko, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo Ibrahim Samwel, Afisa habari na mawasiliano Ali Kamwe, viongozi na wanachama wengine.

"Nichukue nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza sana mashabiki wa Young Africans SC hapa Afrika Kusini. Lakini kwa kipekee niwapongeze sana CRDB kwa ushiriki wao kwenye safari hii ya kuja hapa Afrika Kusini. CRDB Bank wamedhamini safari yetu ya Afrika Kusini, ikiwemo kuleta Mashabiki watano ambao wamejishindia kwenye bahati nasibu ya “Twenzetu kwa Madiba” - Rais wa Young Africans SC Eng.Hersi Said

"Klabu ya Young Africans SC inaendelea kuweka rekodi ya kuzindua matawi nje ya mipaka ya Tanzania. Tumefungua tawi kule nchini DR Congo, na leo tumezindua tawi lingine hapa nchini Afrika Kusini. Tunaposema sisi ni wakubwa tunamaanisha" Ibrahim Samwel - Mkurugenzi wa Masoko, Wanachama na Mashabiki Young Africans SC

Yanga inajiandaa na mchezo dhidi ya Mamelodi Sundwons utakaochezwa kesho ijumaa majira ya saa 3 usiku.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet