Yanga yaandaa Iftar yawaalika Simba na Bodi ya Ligi.
Joyce Shedrack
March 13, 2025
Share :
Klabu ya Yanga imeanda iftar kwa wadau wa soka na kuwaalika Bodi ya Ligi,TFF, na watani wao klabu ya Simba.

"Uongozi wa Yanga umeandaa Iftar kwa Wadau wanaoshirikiana na Yanga hususani wadau wa mpira na lengo kuu ni kuombea mpira wetu kwenye Mwezi huu wa Ramadhan, tumealika Wadhamini Wetu, TFF, Bodi ya Ligi, Kamati ya uendeshaji ya Bodi ya Ligi na Simba SC, zingatio hakuna sehemu ya kucheza mpira ni Iftar tu"
“Kuwaalika Kamati ya Uendeshaji ya Ligi haimanishi tunataka kusawazisha haya yanayoendelea, wala hatutaki kuvunja Msimamo wetu tukio hili ni kwaajili ya Iftar tu sio mambo mengine. Bodi ya Ligi na TFF tumealika kwa lengo jema wala sio mambo ya Mpira na kufturu pamoja haimanishi Msimamo wetu umebadilika”.Amesema Ally Kamwe Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga.