Yanga yaangukia pua Singida Wazir Jr akiibuka shujaa.
Joyce Shedrack
May 13, 2026
Share :
Vinara wa Ligi Kuu Bara, timu ya Yanga imepoteza pambano lake la ligi hiyo dhidi ya Dodoma Jiji kwa kufungwa mabao 3-2.
Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Airtel Stadium Mkoani Singida ulishuhudia Yanga ikipoteza pambano lake la kwanza msimu huu.
Mabao ya Yanga yalifungwa na kiungo wake mshambuliaji Allan Okello aliyefunga mabao mawili, huku mabao ya washindi yakifungwa na Bakari Mwamnyeto aliyejifunga na Mwana Kibuta pamoja na Wazir JR aliyefunga bao la ushindi dakika za mwishobi mwa mchezo.
Matokeo hayo yanafanya mbio za ubingwa kuwa wazi kwa timu za Simba na Yanga, huku Yanga wakiwa na pointi 54, huku Simba wakiwa na pointi 49, lakini Simba wakiwa na mchezo mmoja mkononi.





