pmbet

Yanga yafanya kufuru kwa ankara

Eric Buyanza

December 19, 2023
Share :

Baada ya Yanga kukamilisha usajili wa Shekhan Ibrahim Khamis kutoka Zenji, sasa klabu hiyo yenye makao yake mitaa ya Jangwani, klabu hiyo sasa imehamishia majeshi kwenye kuisaka saini ya mshambuliaji William Karamoko Sankara kutoka klabu ya Asec Mimosa ya nchini Ivory Coast.
 

Mabosi wa Yanga wanamuhitaji mchezaji huyo ili kumtumia hata kwenye michuano ya ndani ikiwemo kutetea mataji mawili ikiwemo FA Cup pamoja na Ligi kuu ya Tanzania Bara.
 

Mkataba wa Sankara na Asec unatamatika mwishoni mwa msimu huu , chanzo chetu cha habari kinatuambia kuna vilabu kutoka Ulaya vimeshaanza kufuatilia sahihi ya mchezaji huyo na hivyo kuifanya kazi hiyo kwa Yanga ya kumsajili kijana huyo wa miaka 20 kuwa ngumu zaidi.
 

Mabosi wa Yanga wameamua kutumia kikamilifu mastaa wa timu hiyo waliopita Asec ili kuweza kumshawishi Sankara ajiunge na timu hiyo na mwenyewe amekubali akiona jamaa zake waliomtangulia wako katika timu salama.
 

Yanga inataka kukamilisha dili hilo kabla ya mwaka huu kutamatika, Rais wa klabu hiyo Engineer Hersi, ndiye masta aliye mbele kwenye vita hii ya kumshawishi Sankara kutia wino Jangwani.
 

Bosi mmoja wa Yanga amesikika akisema kama kuna mchezaji anayewaumiza kichwa kwa sasa basi ni Sankara.

 


 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet