pmbet

Yanga yafungiwa usajili FIFA

Sisti Herman

April 12, 2024
Share :

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia klabu ya Yanga Sc ya Tanzania kusajili wachezaji kwa kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo.

Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imebainisha kuwa Young Africans Sc haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Klabu hiyo imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni, na kuwasilisha taarifa kwa Sekretarieti ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya hatua zaidi.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.

 

ANNEX 3 kwenye kanuni za FIFA za usajili nini? 

 

Annex three ni kipengele cha kanuni kinachozungumzia au kulinganisha usahihi wa taarifa za uhamisho wa mchezaji kwenye mfumo wa usajili yaani Transfer Match System (TMS) ambayo huvitaka vilabu kuweka kwenye TMS taarifa zote za usajili wa mchezaji kama Ada ya uhamisho, Jina lake, Uraia wake.

 

Mfumo huu unaiwezesha TFF, klabu na FIFA kuona taarifa zote za uhamisho wa mchezaji pia inasaidia kumlinda mchezaji, klabu na FIFA.

 

Moja kati ya janga la Dunia wanaloliepuka FIFA kwenye mfumo huu ni utakatishaji fedha kwa kuweka mchezaji hewa ambaye FIFA hawamjui ukasema umemsajili kumbe unapitisha hela kupitia njia hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet