Yanga yafungiwa usajili kisa Kambole
Sisti Herman
April 30, 2024
Share :
Klabu ya Yanga imefungiwa usajili wa kimataifa na shirikisho la soka duniani (FIFA) pamoja na usajili wa ndani na shirikisho la soka nchini (TFF) mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wao Lazarous Kambole raia wa Zambia.
Kambole ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2022-23 kabla ya kutolewa kwa mkopo kwa klabu ya Zesco ya Zambia amefungua kesi aliwashtaki Yanga akidai malimbikizo ya mshahara na fidia ya kuvunja mkataba.