Yanga yaisubiri Simba Robo fainali
Sisti Herman
February 25, 2024
Share :
Mara baada ya ushindi wa magoli 4-0 nyumbani dhidi ya CR Belouizdad kwenye mchezo wa raundi ya 5 ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika kundi D, klabu ya Yanga inakuwa timu ya 6 kufuzu hatua ya robo fainali kati ya 8 zinazohitajika.
Hadi Sasa hizi ndio timu zilizofuzu hatua ya robo Fainali 2023/24 CAF Champions League
Petro Luanda
ASEC Mimosas
TP Mazembe
Al Ahly
Mamelodi Sundowns
Yanga SC
Bado timu 2 tu kukamilisha 8 bora huku nafasi hizo zikiwaniwa na vita ya nafasi ya pili ya kundi B kati ya Simba, Wydad AC na Jwaneng' Galaxy ambao wanamfuatia Asec ambaye amekwishafuzu lakini pia vita ya nafasi ya pili kwenye kundi C kati ya Esperance de Tunis na Al-Hilal.