Yanga yamnasa mrithi wa Feitoto wakiipiku Simba
Eric Buyanza
December 14, 2023
Share :
Taarifa kutoka chanzo cha ndani ya klabu ya Yanga zimethibitisha klabu hiyo kukamilisha usajili wa kiungo wa JKU Shekhan Ibrahim mwenye umri wa miaka 18 tu.
Yanga imemnasa kinda huyo kwa fedha za kitanzania milioni 60 ambazo zitalipwa kwa awamu 3, amesaini mkataba wa miaka mitatu.
Pia inaelezwa kuwa Simba ilikosa nafasi ya kumsajili kiungo huyu dakika za mwisho baada ya kuchelewa kutuma tiketi yake ya ndege.