Yanga yapunguza Adhabu FIFA, bado la Kambole wafunguliwe kusajili
Sisti Herman
June 6, 2024
Share :
Zikiwa zimesalia siku chache kufunguliwa kwa dirisha la Usajili, Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga Sc wamefunguliwa kusajili na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kosa la kushindwa kuweka uthibitisho wa malipo ya usajili wa mchezaji ambaye hajawekwa wazi kwenye mifumo rasmi ya usajili (TMS).
Licha ya kufunguliwa kwa kosa hilo, klabu hiyo itaendelea kusalia kifungoni kwa kosa lingine linalomhusu mchezaji Lazarius Kambole raia wa Zambia ambaye aliwafungulia mashtaka na kushinda kesi dhidi ya Yanga akidai malimbikizo ya mishahara na hela ya usajili.