Yanga yatimiza miaka 89, kuzindua jengo la kisasa jangwani
Sisti Herman
February 5, 2024
Share :
Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amsema kuwa timu hiyo imeanza rasmi wiki ya kuadhimisha ukumbusho wa kuanzishwa na klabu hiyo inayotimiza miaka 89 tangu kunzishwa kwake 1935.
Pamoja na mengi aliyotaja, Kamwe mamesema kawa watazindua jengo la makao makuu ya kisasa ya timu hiyo yaliyopo mitaa ya twiga na jangwani jijini Dar es salaam.
Hizi ni nukuu za Ali Kamwe kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo;
“Leo rasmi tumeingia kwenye wiki ya anniversary ya miaka 89 ya Klabu hii kubwa Tanzania, kuelekea kilele cha Birthday ya Young Africans SC tarehe 11 mwezi huu wa pili, safari hii tuna mambo makubwa. Hii ni wiki yetu wenyewe”
"Kesho Young Africans SC tutakwenda kusaini mkataba na Hospitali kubwa sana duniani, ikiwa na lengo la kumnufaisha shabiki wetu kwenye masuala yanayohusu afya yao. Klabu kubwa lazima iwaze kwa ukubwa namna gani Mwanachama wake atanufaika na Klabu kubwa.
"Siku ya Jumatano, pale makao makuu ya Klabu Jangwani, tunakwenda kuzindua upya ofisi zetu. Uongozi wa Klabu yetu umefanya ukarabati wa kihistoria. Ukarabati huo umeifanya Klabu ya Young Africans SC kuwa na ofisi bora zaidi AFRIKA MASHARIKI NA KATI."
"Ratiba ya tarehe 11 Fabruari tutakuwa Mbeya kwenya mechi dhidi ya Prisons, ambapo birthday yetu itakwenda kufanyika Mbeya. Mkoa wa Mbeya umepata Bahati ya kusheherekea historical Anniversary ya Klabu kubwa katika historia ya mpira wa Tanzania"
"Tunakwenda kuzindua nyimbo mbili kubwa kwa lengo la kusheherekea kilele cha anniversary ya mabingwa wa kihistoria. Yaani kuelekea kwenye hiki kilele ni jiwe juu ya jiwe. Hakupoi, kila mwanachama anapaswa kuweka kambi Mbeya."
"Makamu wa Rais wa Young Africans SC Arafat Haji amenitumia Ujumbe sasahivi kwamba atalipia Basi la waandishi wahabari litakalowapeleka Mbeya na kurudi hii ni kuhakikisha waandishi wanapata matukio yote ya siku hiyo ya kihistoria"