Yanga yawalipa Simba madeni ya Fadlu na wasaidizi wake
Eric Buyanza
November 23, 2026
Share :

Uongozi wa Simba umethibitisha kulipwa fedha walizokuwa wanamdai aliyekuwa kocha wao Fadlu Davis na wasaidizi wake ambao sasa kwa pamoja wamejiunga na Yanga.
Fedha hizo zimelipwa na uongozi wa Yanga ambao ndio waajiri wa makocha hao waliojiunga na kikosi hicho mwanzoni mwa mwezi huu.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amethibitisha taarifa hiyo kwa kuandika “ Tunapenda kuthibitisha kuwa tumepokea malipo ya deni letu kutoka kwa aliyekua Kocha wetu Fadlu Davis yeye pamoja na wasaidizi wake wawili.
“ Deni hilo limelipwa na Mwajiri wake wa sasa. Tunapenda kujipongeza Simba Sports kwa kuwa na nguvu ya kisheria ya kudai deni letu na kulipwa kwa wakati” ameandika Ahmed katika ukurasa wake.





