Yanga yawasili Singida bila Pacome,Job na Damaro.
Joyce Shedrack
March 3, 2026
Share :
Kikosi cha Yanga kimewasili salama Mkoani Singida Jioni ya leo kwa ajili ya mchezo wao wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Singida Black Stars utakaochezwa March 5 kwenye uwanja wa Airtel Stadium.
Katika mchezo huo Yanga watawakosa nyota wao watatu Beki Dickson Job, Kiungo Pacome Zouzoua na Mohamed Damaro.
Dickson Job na Pacome Zouzoua ni majeruhi, Lakini pia Kiungo Mohamed Damaro ametokea kwa mkopo Singida BS hivyo kuna kipengele ambavyo walikubaliana kila wanapokutana mchezaji huyo hawezi kucheza dhidi yao.





