pmbet

Yaya Toure kocha wa kwanza Mwafrika kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Joyce Shedrack

August 27, 2026
Share :

Mchezaji wa zamani wa Ivory Coast na nguli wa soka barani Afrika Yaya Touré, ameweka historia baada ya kuwa kocha wa kwanza Mwafrika kuiongoza timu kufuzu  Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League).

Yaya Touré aiming for Champions League return - AS USA

Touré ambaye aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Slovan Bratislava ya Slovakia mwezi Juni, amekuwa na mwanzo mzuri wa kazi yake baada ya kuisaidia klabu hiyo kutinga hatua awali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

 

Slovan Bratislava ilihakikisha nafasi hiyo usiku wa Jumatano baada ya kuitoa NK Celje ya Slovenia kwa jumla ya mabao 3-2 katika michezo miwili ya mchujo.

 

Kabla ya hapo, Slovan ilianza safari yake ya kufuzu Ligi ya Mabingwa mwezi Julai kwa kuifunga Saburtalo ya Georgia mabao 2-0, kabla ya sare ya 1-1 katika mchezo wa pili.

 

Mbali na mafanikio hayo ya Ulaya, Touré ameanza pia vizuri katika ligi ya ndani, akiiongoza Slovan Bratislava kupata ushindi katika michezo minne ya ligi.

 


 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet