Yaya Toure kufundisha timu ya UEFA CL
Sisti Herman
June 14, 2026
Share :

Kiungo wa zamani wa Manchester City na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Yaya Touré ametangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa klabu ya Slovan Bratislava ya Nchini Slovakia akichukua mikoba ya Vladimir Weiss.
Yaya 43, ambaye pia amewahi kuvichezea vilabu vya Monaco na Barcelona amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuionoa klabu hiyo itakayoshiriki UEFA CL mpaka Juni 2029.
Kabla ya uteuzi huo, Touré alikuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Saudi Arabia kwa kipindi cha miaka miwili na nusu chini ya aliyekuwa kocha mkuu Roberto Mancini.





