Yaya Toure kuinoa timu itakayocheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Joyce Shedrack
June 6, 2026
Share :
Gwiji wa Manchester City Yaya Toure yuko mbioni kuinoa klabu ya Slovan Bratislava ya Ligi Kuu ya nchini Slovakia.

Toure amekubali vipengele vya mkataba wa kuinoa klabu hiyo ambayo msimu ujao itashiriki ligi ya mabingwa Barani Ulaya.
Toure, ambaye alishinda mataji sita akiwa na City yakiwemo mataji matatu ya Ligi Kuu, alistaafu soka ya kulipwa mwaka wa 2019.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast tangu wakati huo amekuwa akijishughulisha na ukocha, na amefanya kazi katika vilabu vingi.
Mnamo Novemba 2023, alijiunga na kocha wa zamani wa City Roberto Mancini kama kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Saudi Arabia.
Alipata rasmi Leseni yake ya UEFA Pro mnamo Januari mwaka jana, na sasa anatazamiwa kuchukua jukumu la kuinoa klabu yake ya kwanza ya kulipwa





