Yoane Wissa azaawadiwa nyumba baada ya kuwafunga kina Ronaldo.
Joyce Shedrack
June 19, 2026
Share :
Mshambuliaji wa DR Congo Yoane Wissa amezawadiwa nyumba ya vyumba vitatu vya kulala katika Jiji la Kinshasa baada ya kufunga dhidi ya Ureno kwenye michuano ya Kombe la Dunia.

DR Congo waliandika historia wakati Wissa alipofunga bao lao la kwanza kabisa katika Kombe la Dunia dhidi ya Ureno na kifanya DR Congo ifanikiwe kuvuna alama moja dhidi ya Ureno.





