pmbet

Yoro ni wa daraja la juu! Rio Ferdinand amtaka Carrick asimuweke benchi

Eric Buyanza

October 20, 2026
Share :

Beki wa zamani na nahodha wa Manchester United F.C., Rio Ferdinand, amemtaka kocha mkuu wa klabu hiyo, Michael Carrick, kuendelea kumuanzisha kikosini beki kijana Leny Yoro, bila kujali ni wachezaji gani waandamizi wanaorejea kutoka kwenye majeraha.

 

Akizungumza kupitia chaneli yake ya YouTube ya Rio Presents, Ferdinand alimsifu sana beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 kwa utulivu na uwezo wake mkubwa wa kuzuia hatari, hasa kwenye mipira ya juu.

 

"Anaonekana kukua kwa kujiamini na sasa anachohitaji ni mfululizo wa mechi kikosini. Sijali ni nani anayerejea kutoka majeraha kwa sasa, nadhani anapaswa kubaki kwenye timu na kuonyesha uwezo wake" alisema Rio.

 

Yoro amekuwa akiongelewa kwa ukubwa katika siku za karibuni baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye timu yake na kwenye timu ya taifa ya  Ufaransa chini ya kocha Zinedine Zidane.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet