Young D atoa tahadhari kuhusu Pombe
Sisti Herman
December 27, 2023
Share :
Msanii wa Hip-Hop, Young D kupitia mitandao yake ya kijamii amewapa tahadhari watumiaji wa baadhi ya pombe zinazotengenezwa nchini Tanzania kwani nyingi zimekuwa hazina ubora na kusababisha magonjwa hatari.
“Wanangu mnaopiga mitungi hapo bongo kuweni makini, kuna pombe nyingi sana feki wakati namiliki bar nilipata shida sana kugundua ipi original, ipi feki. Wagonjwa wa figo wamezidi sana hii miaka miwili kuna viwanda bubu vingi sana hapo mjini” aliandika Young D kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (tweeter)