pmbet

"Yule Najim wa Tabora namkubali sana" - Ambangile

Sisti Herman

May 2, 2024
Share :

Katika tathmini yake baada ya mechi ya kombe la shirikisho CRDBFC kati ya Yanga dhidi ya Tabora United ambapo wananchi Yanga walishinda 3-0, mchambuzi na mwanahabari wavipindi vya michezo wa Wasafi Media, George Ambangile amesema licha ya Tabora kupoteza mchezo kuna baadhi ya wachezaji wao wamemvutia kwa viwango vyao na hata kama wakishuka daraja basi wachezaji hao watabaki kwenye ligi.

"Yule kijana Najim Mussa namkubali" aliandika Ambangile kwenye tathmini yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Najim ambaye anacheza nafasi ya kiungo wa kati amekuwa na kiwango bora huu ukiwa msimu wake wa kwanza kwenye ligi huku akiwa 'panga pangua' kwenye kikosi cha kila kocha anayefika na kundoka kwenye klabu ile tangu ikiwa ligi za madaraja ya chini ikiitwa Kitayosce huku yeye akiwa mmoja wa nyota wachache walioipandisha daraja.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet