pmbet

Zaidi ya mahujaji 500 wafariki kutokana na joto kali

Eric Buyanza

June 19, 2024
Share :

Takribani mahujaji 577 wa mataifa tofauti walikufa walipokuwa wakitekeleza ibada ya Hija ya mwaka huu, wengi wao kutokana na sababu zinazohusiana na joto kali, kulingana na shirika la habari la Ufaransa Agence France-Presse. 

Shirika hilo limewanukuu wanadiplomasia wa Kiarabu kwamba takribani mahujaji 323 wa Misri walifariki walipokuwa wakitekeleza ibada ya Hijja huko Makka. 

Mmoja wa wanadiplomasia wanaoratibu mawasiliano ya nchi zao alisema kuwa "wote walikufa kutokana na joto" isipokuwa mtu mmoja ambaye alijeruhiwa vibaya wakati wa mkanyagano mdogo kati ya umati wa mahujaji, na kuongeza kuwa idadi hiyo ilitoka katika chumba cha maiti cha hospitali ya Al- Muaisem huko Makka. 
Mapema siku ya Jumanne, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilisema kuwa Cairo inashirikiana na mamlaka za Saudia katika kuwatafuta mahujaji wa Misri waliotoweka katika msimu wa Hija. 

Ubalozi mdogo wa Jordan ulitangaza kuwa imetoa vibali 41 vya maziko kwa mahujaji wa Jordan kuzikwa Makka kulingana na matakwa ya familia zao, ikionesha kwamba "hawakuwa sehemu ya ujumbe rasmi wa Hajj wa Jordan. ”

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imesema katika taarifa yake, "Idadi ya mahujaji wa Tunisia waliofariki katika msimu wa Hijja imefikia watu 35 hadi sasa, wakiwemo mahujaji 5 waliofika kupitia mfumo wa bahati nasibu, ambao serikali inaupitisha kuchagua mahujaji kwa kila mwaka, na 30 waliofika kwa ziara, au visa ya Umrah.”

Wizara ya Mambo ya Nje imethibitisha kuwa ujumbe wa kidiplomasia huko Riyadh na Ubalozi mdogo wa Jeddah unashirikiana na mamlaka husika za Saudia na familia za mahujaji kukamilisha taratibu zinazohusiana na maziko yao.

Mamlaka za Saudia ziliripoti kuwatibu zaidi ya mahujaji 2,000 wanaosumbuliwa na uchovu kutokana na joto, lakini hawajatoa maelezo zaidi ya idadi hiyo tangu Jumapili na hawajatoa taarifa kuhusu vifo.
BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet