pmbet

Zaidi ya wahamiaji 500 waokolewa katika nje ya pwani ya Crete, Ugiriki

Eric Buyanza

May 26, 2025
Share :

Zaidi ya wahamiaji 500 kwa jumla, wengi wao wakiwa wanaume, wameokolewa katika siku za hivi karibuni na mamlaka ya Ugiriki katika kisiwa cha kusini cha Crete na kuhamishiwa salama kwenye vituo vya mapokezi, shirika la habari la AFP limesema likinukuu walinzi wa pwani siku ya Jumapili. 

Katika visa vitano tofauti siku nzima ya Jumamosi, jumla ya watu 280 waliokolewa, wakiwemo watoto 13, kulingana na taarifa iliyotolewa siku ya Jumapili.

WENGI WAO WALITOKEA TOBRUK, LIBYA

Operesheni nne zilifanyika karibu na kisiwa kidogo cha Gavdos, kusini mwa Crete mashariki mwa Mediterania. Kisa cha tano kilikuwa kundi la watu 53 ambao walishuka boti lakujazwa kwa upepo huko Dyskos, kusini mwa Crete, siku ya Jumamosi. 

Walisema waliondoka Libya kuelekea Ugiriki siku ya Ijumaa asubuhi, wakilipa "kati ya pauni 150,000 na 200,000 za Misri" (euro 2,600-3,500). Miongoni mwao, mwanamume wa Sudani mwenye umri wa miaka 24, mshukiwa wa wa kusafiriha watu, alikamatwa na kufunguliwa mashtaka. 

Kufikia Ijumaa, jumla ya watu 263 (ikiwa ni pamoja na watoto kumi) waliokolewa katika operesheni tano tofauti katika eneo moja.

Wengi wao walikuwa wameondoka Tobruk, Libya, kuelekea Ugiriki. Wanaume watatu wa Sudani wenye umri kati ya miaka 19 na 23, na Wamisri wawili, ambao umri wao haujatangazwa, washukiwa wa magendo, walifunguliwa mashtaka, kulingana na walinzi wa pwani. 

Miongoni mwa waliookolewa ni raia wa Sudani, Misri na Bangladesh, kulingana na taarifa zao kwa mamlaka ya Ugiriki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet