pmbet

Zaidi ya watu 50 wauawa na waasi wa ADF mashariki mwa Kongo

Eric Buyanza

June 8, 2024
Share :

Zaidi ya watu 50 wameuawa wiki hii katika mashambulizi ya waasi wa ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku watu wengi wakiendelea kuyahama makazi yao. 

Waasi wa ADF wana uhusiano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS, limeua watu 13 katika shambulio kwenye vijiji vitatu huko Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini. 

Hayo yameelezwa na Kinos Katuo, kiongozi wa mashirika ya kiraia katika kitongoji cha Mamove.

Kundi la ADF , ambalo asili yake ni waasi wenye itikadi kali za kiislamu kutoka Uganda, wamekita mizizi kwa karibu miongo mitatu mashariki mwa Kongo. 

Tangu mwaka 2021, majeshi ya Kongo na Uganda yameendesha operesheni za pamoja dhidi ya ADF huko Kivu Kaskazini na Ituri lakini yameshindwa kukomesha mashambulizi dhidi ya raia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet