pmbet

Zaka amvaa Jemedari kuhusu Dabo!

Eric Buyanza

December 6, 2023
Share :

Afisa habari wa Azam Fc Thabity Zakaria "Zaka za Kazi" amemjia juu mchambuzi wa vipindi vya michezo kwenye radio, Jemedari Said kuhusu taarifa anazochapisha kwenye mtandao wake wa kijamii kuhusu kocha wa Azam Fc Youssuf Dabo raia wa Senegal

Anaandika Zaka Zakazi kwenye ukurasa wa instagram;
 

Mchambuzi nguli Jemedari Said amerudia tena kuandika taarifa potoshi kuhusu kocha Yousouph Dabo wa Azam FC. Nasema amerudia tena kwa sababu mara ya kwanza ilikuwa Agosti 13 kwenye ngao ya jamii, alipoandika kwamba Dabo ana Leseni B ya CAF ambayo imeshapitwa na wakati. Na akashangaa kwanini TFF inamuacha anakaa kwenye benchi.
 

Baada ya pale ligi ikaanza na Dabo akakaa kwenye benchi...na zikafuata mechi za CAF, akakaa tena kwenye benchi. Najua Jemedari alimuona Dabo kwenye benchi, ila sijui kama aliendelea kushangaa.
 

Safari hii karudia tena kuandika kuhusu Dabo, akisema 'tuliaminishwa kwambaa ana Pro License.'..mliaminishwa na nani bwana Jemedari? Wewe ndiyo uliaminisha watu kwamba Dabo ana Leseni B ya CAF iliyopitwa na wakati....na hakuna aliyekujibu, siyo Azam FC wala TFF uliowashangaa.
 

Sasa unakuja na hoja nyingine...kwanini lakini meneja wetu wa zamani? Wewe si una access na Azam FC na hata TFF, kwanini usiwaulize ili kubalansi stori?

Ni hivi, wale TFF uliowashangaa, walimuacha Dabo kwenye benchi kwa sababu ana Leseni A ya UEFA. Hii inamfanya atoshe kukaa kwenye benchi bila shida.
 

Na ameipatia Ufaransa katika kituo cha ufundi cha shirikisho la soka la Ufaransa,
Clairefontaine.Yaani kama ni chuo kikuu, basi hiki ndiyo chuo kikuu namba moja cha soka Ufaransa. Kwa sheria na kanuni za Tanzania ambazo zilianzia CAF, ni kwamba kocha mwenye Leseni A ya UEFA akija huku anahesabika sawa na Leseni B.

Na Leseni B haitoshi kuwa kocha mkuu bali msaidizi...ndiyo maana Dabo ameorodheshwa kama kocha msaidizi. Lakini hebu nikuulize kitu Bin Kazumari.
 

Hivi wewe unaweza kuwa na shaka na mtu mwenye elimu ya kutoka chuo kikuu namba moja katika nchi kama Ufaransa? Yaani tuseme wewe una hospitali yako na unaajiri madaktari bingwa halafu anakuja daktari bingwa aliyepata first class degree ya chuo kikuu namba moja cha Ufaransa, utakuwa na shaka naye?
 

Au mwanao amemaliza form six na akapata scholarship kwenda kusoma chuo kikuu namba moja Ufaransa, utakuwa na mashaka kuhusu elimu atakayopata? Anyway, kila mtu anaweza kuwa na majibu yake, lakini ukweli ni kwamba haikukawahi kutangazwa popote kwamba Dabo ana Pro License! Dabo ana Leseni A ya UEFA!

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet