Zaku-scan zimeanza kutolewa feki Simba yatoa onyo.
Joyce Shedrack
September 18, 2025
Share :
Uongozi wa klabu ya Simba kwa kushirikiana na mzabuni wa jezi na vifaa vya michezo Kampuni ya Jayrutty Investment East Africa Limited umebaini kuwepo kwa jezi feki za Simba zilizosambazwa mikoani, hususani mikoa ya Morogoro, Singida, Mwanza, na Geita.
Ugunduzi huo umetokana na operesheni maalum iliyofanywa kwa msaada wa Jeshi la Polisi na tayari baadhi ya wahusika wamekamatwa kwa hatua kali za kisheria dhidi yao.
Simba inasisitiza kwamba uzalishaji, uuzaji, usambazaji na utumiaji wa jezi na bidhaa feki ambazo hazijazalishwa na Jayrutty Investment ni kosa kisheria na hatua kali za kisheria (Madai na Jinai) zitachukuliwa kwa yeyoye atakayethubutu kuzalisha, kuuza, kusambaza ama kutumia jezi na bidhaa feki kwani vitendo hivyo ni uhujumu wa wazi dhidi ya klabu.
Ulinzi mkali utakuwepo maeneo yote nchi nzima kudhibiti na kukamata wahusika wote na bidhaa feki.
Klabu inatoa rai kwa wanasimba na raia wote kutoshiriki katika matumizi ya bidhaa feki na mtu yeyote atakayebaini uwepo wa jezi na bidhaa feki mahala popote atoe taarifa kituo chochote cha Polisi na/ama kupiga Simu zifuatazo
1. 0752 111 181
2. 0784 128 220
3. 0742 771 311
Zawadi nono itatolewa kwa watakatoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa jezi feki.