Zamira anywa sumu ya panya, baada ya kulazimishwa kuolewa na mtu asiyemtaka
Eric Buyanza
February 19, 2024
Share :
Mkazi wa kijiji na kata ya Makote wilayani Newala, Zamira Mohamed amekunywa sumu ya panya aina ya rotax na kujikata na wembe kwenye mguu wake wa kulia kwa lengo la kutaka kujiua.
Zamira ambaye pia ana mtoto wa mwaka mmoja alifanya maamuzi hayo baada ya kulazimishwa kuolewa na mtu ambaye hamtaki.
Baada ya tukio hilo alipoteza fahamu kisha kufikishwa katika hospitali ambapo mpaka sasa anaendelea kupatiwa matibabu.