pmbet

Zanzibar kujenga mji wa Serikali

Sisti Herman

August 13, 2025
Share :

 

Kamati ya wataalamu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Dkt. Islam Seif Salum, leo Agosti 12, 2025, imetembelea miradi mikubwa katika Jiji la Dodoma.

Miradi hiyo ni pamoja na Mji wa Serikali wa Mtumba na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, kwa lengo la kujifunza kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa Mji wa Serikali.

Ziara hiyo inalenga kuandaa mazingira kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Serikali na Baraza la Wawakilishi katika eneo la Kisakasaka, Zanzibar.

Viongozi hao wametoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuimarisha maendeleo ya Makao Makuu ya nchi kupitia miradi ya kimkakati.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet