pmbet

Zari kuwafukuza watoto wake nyumbani

Sisti Herman

December 18, 2023
Share :

Mjasiriamali maarufu wa Uganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Zari The Boss Lady amefichua mipango ya kuwafukuza vijana wake watatu aliozaa na marehemu mume wake, Ivan Ssemwanga kutoka nyumbani kwake ili kwenda nje kujitafutia maisha yao.

Zari alifichua mipango hiyo katika video moja aliyoposti kwenye TikTok akihojiwa ambapo alisema kwamba kwa sasa wanawe hao ni watu wazima ambao wanafaa kuanza kujitafutia maisha na sio tu kuendelea kulelewa na mama yao wakati wameshazidi miaka 18.

Zari alisema kwamba kinachomchochea zaidi kuwafukuza nyumbani kwake ni baada ya video ya hivi karibuni ambayo iliwaonesha wakipigania nafasi ya kuegesha magari kila mmoja akitaka kuliegesha gari lake kwenye nafasi hiyohiyo moja.

"Bado tunapigana kuhusu maegesho katika yadi yangu, lakini natumai, wavulana wangu watahama mwaka ujao. Wanamiliki vyumba na magari na wanahitaji kwenda. Wanahitaji tu kwenda. Kwa hivyo tunatumai kuwa hilo litapangwa mwaka ujao," alisema.

Zari ni mama wa watoto 5, watatu wa kwanza ambao ni watu wazima sasa wakiwa wote ni wavulana aliozaa na marehemu mumewe Ivan Semwanga huku wadogo wawili akizaa na msanii Diamond Platnumz kati ya mwaka 2015 na 2018 kabla ya kuachana.

Kwa sasa, mama huyo anaishi na mpenzi wake mdogo, Shakib Lutaaya Cham ambaye walifunga ndoa ya Kiislam mwezi Aprili mwaka huu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet