pmbet

Zawadi ya Bilioni 26 kutolewa kwa atakayetoa taarifa za kukamatwa kwa hawa - Marekani

Eric Buyanza

August 25, 2026
Share :

Serikali ya Marekani imetangaza zawadi ya hadi dola milioni 10 za Kimarekani (zaidi ya Shilingi bilioni 26 za Kitanzania) kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kuwatambua au kuwatafuta viongozi wakuu na makamanda wa Jeshi la Mapinduzi la Iran (IRGC).
 

Tangazo hili limetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na linalenga hasa viongozi wanaotuhumiwa kupanga na kusimamia vitendo vya kigaidi na mashambulizi ya kimtandao dhidi ya maslahi ya Marekani.

 

Marekani imetaja orodha ya viongozi kadhaa wa ngazi za juu wa kisiasa na kijeshi wanaotafutwa kuwa ni;
 

Ayatollah Mojtaba Khamenei:

Kiongozi Mkuu mpya wa Iran (mtoto wa aliyekuwa Kiongozi Mkuu, Ali Khamenei).
 

Ahmad Vahidi:

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Mapinduzi (IRGC).
 

Ali Abdollahi:

Mkuu wa Makao Makuu ya Ulinzi ya Khatam al-Anbiya.

 

Saeed Aghajani:

Kamanda wa Kitengo cha Ndege zisizo na Rubani (Drones) za Jeshi la IRGC.

 

Hamidreza Lashgarian:

Mkuu wa Kitengo cha Mashambulizi na Ulinzi wa Kimtandao (Cyber-Electronic Command) wa IRGC.
 

Majid Khademi:

Kamanda wa Ofisi ya Idara ya Ujasusi ya IRGC.
 

Mbali na kiasi hicho cha fedha, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeeleza kuwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za kuaminika na zinazofaa anaweza pia kufanyiwa mchakato wa kuhamishwa na kupewa makazi mapya kwa usalama nje ya nchi hiyo pamoja na familia yake ili kulinda usalama wake.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet