Zelensky amfuta kazi kamanda mkuu wa jeshi la ukraine
Eric Buyanza
February 9, 2024
Share :
Rais wa Ukraine amemfuta kazi kamanda mkuu wa jeshi la nchi hiyo Valerii Zaluzhnyi.
Hatua hii inafuatia uvumi kuhusu mpasuko kati ya rais na Jenerali Zaluzhnyi, ambaye ameongoza juhudi za vita vya Ukraine tangu mzozo huo uanze.
Jenerali Oleksandr Syrskyi alitangazwa kuchukua nafasi yake katika agizo la rais.
Ni mabadiliko makubwa zaidi kwa uongozi wa kijeshi wa Ukraine tangu uvamizi kamili wa Urusi mnamo Februari 2022.
Rais Volodymyr Zelensky alisema....."Kuanzia leo, timu mpya ya usimamizi itachukua uongozi wa Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine."
Jenerali Zaluzhnyi ni maarufu na anayeaminiwa na wanajeshi wa Ukraine na umma, na amekuwa shujaa wa taifa.
Katika siku za hivi karibuni, makadirio ya kukubalika kwake yamekuwa ya juu kuliko yale ya Bw Zelensky.
Rais alisema yeye na Jenerali Zaluzhnyi walikuwa na "mazungumzo ya wazi" kuhusu mabadiliko yanayohitajika katika jeshi, na kwamba alimshukuru jenerali kwa kuilinda Ukraine dhidi ya Urusi.