Zelensky amfuta kazi mkuu wa ulinzi baada ya kukosakosa kuuawa
Eric Buyanza
May 11, 2024
Share :
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfuta kazi mkuu wa idara inayohusika na ulinzi wake, baada ya maafisa wawili katika idara hiyo kukamatwa wiki hii kuhusiana na madai ya jaribio la kutaka kumuua rais huyo
Amri ya Zelenskiy ya kumwachisha kazi Sergiy Leonidovich Rud haikutaja sababu ya hatua hiyo wala mtu atakayeichukua nafasi yake katika wadhfa huo wenye umuhimu mkubwa.
Tangazo hilo limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya idara ya usalama ya Ukraine SBU kutangaza kwamba, imezima jaribio la Urusi la kumuua Zelenskiy na maafisa wengine waandamizi serikalini. SBU iliongeza kuwa inawashikilia makanali wawili inaowashuku walivujisha taarifa kwa shirika la usalama la Urusi FSB.