pmbet

Zelensky amuita Putin ‘Muuaji’ baada ya Trump kumuita ‘Rafiki’

Eric Buyanza

November 21, 2026
Share :

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amemshutumu vikali Rais wa Urusi, Vladimir Putin, akimwita "muuaji" , siku chache baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kumtaja kiongozi huyo wa Urusi kuwa ni "rafiki" yake wakati wa mkutano wao nchini China.

 

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN, Zelensky alisema kuwa ni uamuzi wa Rais Trump jinsi anavyopenda kumwita Putin, lakini kwa upande wa Ukraine ukweli uko wazi.

 

"Kwetu sisi, yeye ni adui. Na bila shaka, kwetu sisi yeye ni muuaji. Nadhani hata kwa watu wengi duniani, yeye ni muuaji kwa sababu anaua watu kila siku na kila usiku," alisema Zelensky. Aliongeza kuwa kumtaja Putin kama rafiki kunapunguza shinikizo la kimataifa dhidi yake.

 

Msimamo huo wa Zelensky unakuja huku gazeti la Ukraine la European Pravda likiripoti kuwa kiongozi huyo ameonya kwamba kumwita Putin "rafiki" kunampa kiburi na kupunguza shinikizo la kimataifa analopaswa kuwekewa. Hata hivyo, Zelensky alikiri kuwa Marekani bado inabaki kuwa mpatanishi mwenye nguvu zaidi anayeweza kumsukuma Putin mezani kwa mazungumzo ya amani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet