pmbet

Zelensky aomba ruhusa ya kuipiga urusi kwa makombora ya magharibi

Eric Buyanza

July 19, 2024
Share :

Katika mkutano na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na baraza lake la mawaziri, Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky kwa mara nyingine tena, ametoa wito kwa washirika kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za Magharibi katika ardhi ya Urusi.

"Muhimu kwa hili ni silaha za masafa marefu. Tafadhali washawishi washirika wetu wengine kuondoa vizuizi, "Zelensky alimueleza Bw Starmer, akimaanisha kuruhusu mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa silaha za Magharibi kwenye eneo linalotambuliwa la Urusi bila vizuizi.

Alipopokelewa na mwenyeji wake katika makazi ya Waziri mkuu wa Uingereza, Zelensky aliishukuru Uingereza kwa msaada na mshikamano wake na Ukraine.
“Asante kwa mwaliko na kunipa heshima ya kuwa hapa. Asante kwa umoja huu. 

Tunahisi msaada huu, na maamuzi yako mazito yalisaidia kulinda uhuru na demokrasia nchini Ukraine na kuwasaidia sana watu wa Ukraine’’ , amesema na kuongeza kuwa "Pia nataka kujadili na wewe leo maamuzi mazito ambayo yanaweza kutusaidia katika vita hivi," Zelensky aliongeza.

Rais wa Ukraine amekuwa mgeni wa kwanza wa kigeni tangu Starmer achaguliwe kama waziri mkuu mpya. 
BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet