Zelensky atambishia mifumo ya Patriot itakayopelekwa Ukraine
Eric Buyanza
June 12, 2024
Share :
Rais wa Ukraine, Vladimir Zelensky, ambaye yuko ziarani nchini Ujerumani,amechapisha picha ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Patriot, ambao utapelekwa Ukraine.
Akiwa kwenye ziara hiyo Zelensky alitembelea kambi ya kijeshi katika mji wa Zanitsa akiongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius na pia aliishukuru nchi hiyo kwa kifurushi kipya cha msaada chenye thamani ya Euro milioni 700.
Zelensky pia amebainisha kuwa jeshi la Ukraine litapokea sio tu mfumo mwingine wa ulinzi wa anga wa Patriot, lakini pia mifumo ya hali ya juu ya IRIS-T iliyotengenezwa na Ujerumani.
Katikati ya mwezi Aprili, baada ya Urusi kuzidisha mashambulizi yake ya makombora dhidi ya miji ya Ukraine, Ujerumani ilikubali kuhamisha mfumo mwingine wa Patriot kwenda Ukraine.
Zelensky hapo awali aliwaambia washirika wa NATO kwamba takriban mifumo saba zaidi ya Patriot inahitajika ili kuilinda miji ya Ukraine dhidi ya makombora ya Urusi.