pmbet

Zidane angependelea zaidi kufundisha Man United kuliko Bayern Munich

Eric Buyanza

April 20, 2024
Share :

Kulingana na jarida la 'L'Equipe' la nchini Ufaransa, kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane angependelea zaidi kuhamia Old Trafford badala ya Allianz Arena.

Inaelezwa kuwa Zidane anaisheshimu klabu hiyo ya Ujerumani, lakini anaona lugha pamoja na maisha kwenye kitongoji cha Bavaria ilipo maskani ya timu hiyo kuwa kikwazo kikubwa.

Zidane ni mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi kwenye zama hizi akiwa na Real Madrid, akishinda Ligi ya Mabingwa misimu mitatu mfululizo, bila kusahau kubeba ubingwa wa La Liga mara mbili, kuchukua Kombe la UEFA Super Cup, na kubeba kombe la Dunia la Vilabu la FIFA mara mbili. 

Licha ya kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yake ya ukocha, Zidane ameifundisha Real Madrid pekee.

Kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 51, hajapata kazi tangu 2021. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet