Zidane Iqbal wa Iraq kuandika historia kwenye kombe la dunia
Eric Buyanza
June 16, 2026
Share :

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Zidane Iqbal anataraji kuweka historia ya Kombe la Dunia ikiwa atapangwa kuichezea Iraq dhidi ya Norway Jumatano Juni 17, lakini itakuwa historia kubwa kwa nchi ya Pakistani.
Pakistan, taifa la zaidi ya watu milioni 240, likishika namba tano kwa idadi ya watu Duniani, ambapo timu yao ya soka ya Taifa haijawahi kucheza fainali za Kombe la Dunia.
Zidane anayekipiga na Utrecht ya nchini Uholanzi, licha ya kuichezea Iraq, atakuwa mchezaji wa kwanza wa asili wa Pakistani kucheza Kombe la Dunia la Wanaume.
Iqbal alizaliwa na kukulia huko Manchester, nchini Uingereza,lakini amefata uraia wa Iraq kwenye uzao wa mama yake na baba yake ni mzaliwa wa Pakistan.
Kiungo huyo mwenye kipawa anasema anajivunia kuwakilisha mataifa yote mawili na anaonyesha hivyo anapoingia uwanjani kwa kuvaa bendera za nchi zote mbili kwenye viatu vyake.





