Zidane kumrithi Deschamps Ufaransa
Sisti Herman
March 23, 2026
Share :

Baada ya kusubiri kwa siku 1,727 bila ajira, fundi Zinedine Zidane anaripotiwa kufikia makubaliano ya mdomo na Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) kuwa kocha mkuu ajaye wa "Les Bleus".
Zizou anatarajiwa kumrithi Didier Deschamps mara baada ya fainali za Kombe la Dunia 2026. Rais wa FFF, Philippe Diallo, amethibitisha kuwa tayari anajua nani atakuwa bosi mpya wa timu hiyo.
Deschamps, ambaye amekuwa kileleni tangu 2012 na kuipa nchi hiyo Kombe la Dunia 2018, ameweka wazi kuwa safari yake itafika kikomo mwaka 2026. "Lazima ifike mwisho wakati fulani," alisema Deschamps.





