Zidane, Messi na Iniesta ni wachezaji wangu bora wa muda wote - Rodri
Eric Buyanza
July 29, 2026
Share :
Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri amewataja wachezaji wake watatu bora wa muda wote.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na Sports Direct, kiungo huyo aliombwa kutaja wachezaji anaowapenda zaidi wa wakati wote.

Bila kusita, Rodri aliwataja gwiji wa Real Madrid Zinedine Zidane, nahodha wa Argentina Lionel Messi, na fundi wa zamani wa kiungo wa Barcelona, Andres Iniesta.





