Zijue njia tano za kulinda figo zako
Eric Buyanza
March 16, 2024
Share :
KUNYWA MAJI MENGI KWA SIKU
Kunywa angalau glass 8 za maji kwa siku, maji yatalinda figo, haswa kwa wagonjwa walio na hatarini kama vile wagonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, ugonjwa wa seli mundu.
PUNGUZA UNYWAJI POMBE / ACHA SIGARA
Kupunguza au kuacha kabisa pombe na sigara ni muhimu ili kuziweka figo zako katika hali ya usalama. Pombe na sigara ni maadui wa figo.
TUMIA DAWA KWA USAHIHI
Unapaswa kumuuliza daktari wako kuhusu matumizi ya dawa. Baadhi ya dawa zinaweza kuharibu viungo vyako, hasa figo. Tafuta ushauri wa matibabu na usinunue dawa mtaani.
FANYA VIPIMO
Kitu kingine ambacho kila mtu anapaswa kufanya, ni vipimo vya tumbo angalau mara moja kila baada ya miaka miwili hadi mitano. Ili kuangalia afya ya figo na viungo vingine.
FANYA MAZOEZI
Tumia dakika 30 au zaidi kwa siku kufanya mazoezi. Husaidia kurekebisha kalori zako na kubaki katika uzito mzuri.