ZIJUE SHERIA ZA TALIBAN KWA WANAUME: Marufuku kuvaa Tai, kunyoa panki au kunyoa ndevu
Eric Buyanza
August 31, 2024
Share :
Sheria hizi mpya ni maalum kwa wanaume
* Sasa wanaume wanatakiwa kufunika miili yao kuanzia kwenye kitovu hadi magotini wakiwa nje ya nyumba zao, kwani sehemu hizi za mwili huchukuliwa kuwa ni 'awrah' yaani (Utupu).
* Wanaume hawaruhusiwi kutengeneza nywele zao (kunyoa style) kwa njia ambayo ni kinyume na sharia.
* Taliban imepiga marufuku vinyozi katika majimbo kadhaa kunyoa au kupunguza ndevu, kwa madai kwamba amri hii inaambatana na sharia.
* Sheria ya maadili pia inakataza wanaume kuvaa tai.