Zimbabwe kuanza kutumia VAR kwenye ligi yao
Sisti Herman
November 12, 2026
Share :

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zimbabwe (ZIFA) lipo katika hatua za mwisho za kuanzisha matumizi ya teknolojia ya mfumo wa usaidizi wa video (VAR) katika soka la nchi hiyo.
Tayari, mafunzo ya matumizi ya mashine hizo yanaendelea ambapo mifumo hiyo inatarajiwa kuanza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye fainali ya Chibuku Super Cup inayotarajiwa kufanyika Novemba 2026.





