Zingatieni usalama wenu wakati wa uchimbaji dhahabu
Eric Buyanza
April 29, 2026
Share :

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limewataka wachimbaji wa dhahabu machimbo ya Nyamwilonge kata ya Nyamtukuza, Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kuchukua tahadhali wanapokuwa katika shughuli ya uchimbaji wa madini kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Tahadhali hiyo imetolewa April 28, 2026 na Mkaguzi wa Polisi (INSP) Emmanuel Nzunda wakati akitoa elimu ya usalama maeneo ya kazi ambapo amewataka wachimbaji hao kulinda usalama wao kwa kuchukua tahadhali muhimu.
INSP Nzunda amewataka wachimbaji hao kutowatumia watoto kwenye shughuli za uchimbaji kwani watoto hao wanakosa haki ya msingi ikiwemo kupata elimu.
Pamoja na hayo amewataka wachimbaji hao wa madini kuendelea kutoa taarifa ya uhalifu na wahalifu ili wachukuliwe hatua za kisheria.
@polisi.tanzania





