Ziwa Tanganyika kufungwa kwa miezi mitatu, Lipumzike
Eric Buyanza
April 3, 2024
Share :
Shughuli za Uvuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma zinatarajiwa kufungwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Mei 15 hadi Agosti 15, mwaka huu lengo likiwa ni kupumzisha ziwa hilo kupata ongezeko la samaki.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kukuza sekta ya Uvuvi nchini kwa kusaidia ongezeko la samaki ziwani humo.